GET INVOLVED
Young Life ipo ili kuwajulisha vijana kuhusu Yesu Kristo na kuwasaidia kukua katika imani yao. Young Life inajihusisha na watoto wenye umri wa kuwa katika shule ya msingi, shule ya sekondari na chuo katika majimbo yote 50 ya Marekani pamoja na zaidi ya nchi 90 duniani.
Ili kuendeleza misheni hii ya ulimwenguni, Young Life na mashirika yake mbalimbali ya uchunganji (Young Life) huenda wakusanye, wachakate, watumie, na wapeane taarifa yako ya kibinafsi. Kauli hii ya Faragha imeandikwa ili kukuelezea jinsi ambavyo huenda Young Life itumie taarifa yako ya kibinafsi na jinsi ambavyo Young Life inathamini wajibu wake kwako wa kulinda haki zako na taarifa yako ya kibinasfi.
Katika sehemu ambazo tunatumia maneno “Young Life,” “tu,” “sisi,” na “yetu,” tunamaanisha Young Life, shirika lisilo la faida la Texas, na tanzu zake na mashirika yanayoshirikiana nayo. “Taarifa ya Kibinafsi” kwa kawaida humaanisha data zote ambazo zinakuhusu moja kwa moja au zisizo kuhusu moja kwa moja, lakini “taarifa ya kibinafsi,” “data ya kibinafsi,” au “taarifa inayoweza kukutambulisha” na maneno mengine huenda yakahusika kulingana na sheria inayotumika na yatakuwa na maana ya sheria hizo zinazohusika.
Mara kwa mara, huenda tusasishe Kauli hii ya Faragha, kwa hivyo tunakuhimiza upitie upya kauli hii mara kwa mara, huku ukizingatia kwa makini tarehe ambayo “ILISASISHWA MWISHO” iliyopo hapo juu. Katika hali fulani, huenda Young Life iwasiliane na wewe ili kukujulisha haswa kuhusu mabadiliko ya Kauli hii ya Faragha.
Ni sera ya ulimwenguni ya Young Life ya kuwa makini sana inaposhughulikia taarifa ya kibinafsi inayokusanya, inayochakata, inayotumia, na inayopeana. Young Life itadumisha sera na michakato inayofaa katika misheni ya ulimwenguni ili kuzidisha ulinzi wa data ya kibinafsi na kuhakikisha inafuata sheria na kanuni zinazotumika. Young Life pia imejituma kupitia upya na kuongeza sera na michakato hii mara kwa mara kama sehemu ya Mpango wake wa Faragha wa Ulimwenguni.
Young Life ni shirika la ulimwenguni linalodumisha sera na shughuli za ulinzi wa data zinazoambatana na kanuni zinazokubalika kimataifa za faragha ya data. Sera hizi zinaongezea sheria za faragha ya data ya kitaifa, na sheria yoyote ya kitaifa hupewa kipaumbele endapo inagongana na sera za Young Life. Ulaya, Sheria ya Ulinzi ya Takwimu ya Jumla (GDPR) ilianza kutumika kuanzia tarehe 25 Mei, 2018. Ikiwa GDPR na/au sheria nyingine za faragha za EU zinakuhusu, Kauli hii ya Faragha inaelezea jinsi ambavyo unaweza kutumia haki zako.
Young Life hukusanya aina zifuatazo za taarifa ya kibinafsi:
Taarifa ya mawasiliano: Inajumuisha nambari ya simu, anwani, UJUMBE MFUPI, anwani ya barua pepe, nambari ya simu, maelezo mafupi ya mitandao ya kijamii
Demografia: Inajumuisha taarifa kukuhusu, unapoishi, na mipango na shughuli ambazo huenda ukapenda katika Young Life
Taarifa ya ajira: Inajumuisha taarifa inayohitajika kushughulikia ombi lako la ajira na kukamilisha mchakato wako wa kuelekeza mwajiriwa, kama vile kazi ulizofanya hapo awali, wadhamini, historia ya kufungwa jela kwa kesi ya jinai, sifa za kipekee au kazi unazopendelea
Historia ya Kifedha: Inajumuisha taarifa ya utoaji wako wa msaada au mchango kwa Young Life, huduma au bidhaa ulizonunua kutoka kwa Young Life, shughuli nyingine za kifedha ambazo umeshafanya na Young Life
Data ya Utambulisho: Inajumuisha jina, tarehe ya kuzaliwa, jinsia, hali ya ndoa
Taarifa kuhusu Imani Yako: Inajumuisha taarifa kuhusu dini
Taarifa ya Malipo: Inajumuisha nambari za akaunti ya benki na za kutambulisha benki, nambari za kadi ya mkopo/kadi ya benki, nambari ya hundi, maelezo mengine muhimu ya kifedha
Maombi na Mapendeleo: Inajumuisha jinsi ambavyo ungependa Young Life iwasiliane na wewe, mabadiliko ambayo umefanya katika akunti yoyote ya Young Life
Data ya Afya Inayohitajika: Inajumuisha taarifa ya afya ambayo Young Life inahitaji ili uweze kuhudhuria kambi ya Young Life au kushiriki katika safari au tukio la Young Life, ikiwemo historia ya matibabu, rekodi za chanjo, rekodi za daktari, na vipimo vya kibiolojia
Hati za Utambulisho wa Usalama: Inajumuisha taarifa ya kuingia na nenosiri
Taarifa ya Kusafiri: Inajumuisha maombi yanayohusiana na safari zako na Young Life, taarifa ya pasipoti, vyakula unavyohitaji kula au usivyofaa kula
Taarifa kuhusu Kujitolea: Inajumuisha taarifa inayohitajika kushughulikia ombi lako la kujitolea na kukamilisha mchakato wako wa kujiunga, ikiwemo wadhamini, historia ya kufungwa jela kwa kesi ya jinai, sifa za kipekee
Taarifa ya Young Life: Inajumuisha taarifa kuhusu historia na kujihusisha kwako na Young Life
Young Life hutumia taarifa ya kibinafsi unayopeana ili kushughulikia vyema maombi yako na kukuunganisha zaidi na shughuli za misheni na uchungaji za Young Life. Ikiwa unahusika katika mpango wa klabu au kambi ya Young Life au unatoa muda na/pesa yako kwa malengo yetu ya misheni, Young Life itatumia taarifa yako ya kibinafsi kutimiza maslahi yake halali yanayohusiana na misheni ya shirika letu. Hatuuzi, kukodisha au kupea watu wengine taarifa yako ya kibinafsi. Young Life itachakata tu taarifa yako ya kibinafsi kulingana na msingi unaofaa wa kisheria na kwa sababu tu zilizoelezwa katika Kauli hii ya Faragha. Jedwali lililo hapa chini linatoa orodha ya mifano ya jinsi ambavyo huenda tukatumia taarifa yako, aina za taarifa zinazohusika, na msingi wa kisheria wa sisi kutumia taarifa yako.
Jinsi Ambavyo Tunatumia Taarifa Yako ya Kibinafsi
Aina za Taarifa za Kibinafsi Zinazohusika
Msingi wa Kisheria
Mifano na Maelezo
Kuwasiliana na wewe kuhusu taarifa inayohusu shughuli za uchungaji ambazo Young Life inatoa katika eneo lako
Data ya utambulisho, Taarifa ya mawasiliano
Maslahi Halali
Huenda mfanyakazi au mtu anayejitolea wa Young Life atumie jina au nambari yako ya simu kukualika kwenye shughuli ya klabu ya Young Life iliyoko katika eneo lako.
Kukuwezesha uhudhurie kambi ya Young Life na kufuatilia baada ya mahudhurio
Data ya utambulisho, Taarifa ya mawasiliano, Data ya Afya Inayohitajika, Maombi na Mapendeleo, Demografia, Taarifa ya Malipo, Taarifa ya Usafiri
Mkataba
Tunafikiria kwamba utakuwa na wiki bora sana katika maisha yako ukihudhuria kambi ya Young Life. Tutahitaji taarifa fulani kutoka kwa watoto na wazazi ili kurahisisha tukio la kambi.
Kurahisisha kushiriki kwako katika safari ya Young Life
Data ya utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Data ya Afya Inayohitajika, Maombi na Mapendeleo, Demografia, Taarifa ya Malipo, Taarifa ya Usafir
Mkataba
Young Life ina baadhi ya safari nzuri za misheni za muda mfupi, lakini tunahitaji taarifa ya kibinafsi ili itusaidie kupanga safari na kuwasiliana kuhusu habari muhimu ya safari.
Kukusaidia kuunda akaunti katika mtandao wa Young Life
Data ya utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Maombi na Mapendeleo, Demografia, Hati za Utambulisho wa usalama
Mkataba na Maslahi Halali
Ikiwa unahudhuria mojawapo ya matukio yetu au wewe ni mfadhali wa Young Life, tunataka uweze kujihusisha na sisi kwa urahisi. Kwa hivyo, tunatumia mitandao tofauti kuzidisha utakayopitia katika Young Life.
Kwa mawasiliano ya mauzo ya kielektroniki yanayohusiana na shughuli za uchungaji za Young Life au yanayohusiana na nafasi za kutoa msaada kwa Young Life
Data ya utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano
Idhini au Maslahi Halali
Tunapenda kukujulisha kuhusu nafasi za Young Life ambazo huenda bado hujui, lakini hatutaki kukutumia mawasiliano ambayo hutaki. Ikiwa umeshashirikiana na sisi hapo awali, tunaamini kwamba tunaweza kuwasiliana na wewe kuhusu mawasiliano ya mauzo ya kieletroniki. Hata hivyo, tunataka usimamie mambo, kwa hivyo tafadhali tujulishe ikiwa hutaki kuendelea kupokea aina hii ya taarifa.
Kwa mawasiliano yasiyo ya mazungumzo (k.m. barua, simu, nk.) yanayohusiana na shughuli za Young Life
Data ya utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano
Maslahi Halali
Bado huwa tunatumia huduma ya barua mara kwa mara kuwasiliana na wewe kuhusu kujihusisha kwako katika Young Life na kukujulisha kuhusu mambo mapya muhimu kuhusu kazi yetu ya watoto.
Kwa mawasiliano ya kielektroniki yasiyo ya mauzo kukujulisha kuhusu habari na mambo mapya ya Young Life
Data ya utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano
Maslahi Halali
Wafanyakazi wetu hujulisha wanaotaka kuwa wafadhili na marafiki kuhusu hadithi na habari kuhusu mambo ambayo wanafanya katika kazi zao.
Kukuruhusu utume ombi la kutoa huduma kwa Young Life kama mfanyakazi au mtu ajitoaye
Data ya Utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Taarifa kuhusu Imani yako, Maombi na Mapendeleo, Hati za Utambulisho wa Usalama, Demografia, Taarifa ya Young Life
Mkataba
Young Life huchunguza wanaoweza kuwa wafanyakazi na watu wajitoao kwa makini ili kuhakikisha kwamba wanaweza kujiunga na kazi yetu ya watoto.
Kurahisisha uandikishaji wako katika shughuli ya kuchangisha fedha ya Young Life na kufuatilia baada ya tukio
Data ya Utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Taarifa ya Malipo
Mkataba
Huenda mfanyakazi au mtu anayejitolea wa Young Life akualike ujiunge na mashindano ya gofu au dhifa ili ujifunze mengi na uunge mkono kazi ya Young Life katika eneo lako.
Kwa usimamizi wa wawasiliani
Data ya Utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Maombi na Mapendeleo, Demografia
Maslahi Halali
Tunafanya kazi kwa bidii ili kusimamia taarifa yako ndani ya mfumo wetu kwa njia inayofaa zaidi ili tuweze kujibu maombi yako haraka yanayohusiana na Young Life au yanayohusiana na haki zako au taarifa ya kibinafsi.
Kutoa huduma za uchungaji kama vile mwongozo wa kiroho au Shauri la kibiblia
Data ya Utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Taarifa kuhusu Imani yako
Maslahi Halali
Tunaamini kwamba Mungu anakupenda na Mungu anapenda watoto, na wafanyakazi wetu na watu wanaojitolea wanataka kuwa katika maisha ya watoto ili kusikia wanayopitia na kuonyesha upendo wa Kristo.
Kukuajiri kama Mfanyakazi wa Young Life
Data ya Utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Taarifa kuhusu Imani yako, Maombi na Mapendeleo, Hati za Utambulisho wa Usalama, Demografia, Taarifa ya Ajira
Mkataba na Wajibu wa Kisheria
Ili ufanyie Young Life kazi, lazima utoe taarifa fulani ya kibinafsi ili kurahisisha ajira yako.
Kurahisisha shughuli yako ya kujitolea katika Young Life
Data ya Utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Taarifa kuhusu Imani yako, Maombi na Mapendeleo, Hati za Utambulisho wa Usalama, Demografia, Taarifa ya Kujitolea
Mkataba na Wajibu wa Kisheria
Ili ujitolee katika Young Life, lazima utoe taarifa fulani ya kibinafsi ili urahisishe kujitolea kwako.
Kushughulikia mchango wako
Data ya Utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Taarifa ya Malipo
Mkataba na Wajibu wa Kisheria
Unapotolea Young Life mchango, tutakuomba utoe taarifa inayohitajika ili kukamilisha mchango wako na kuunda rekodi zinazofaa.
Kwa wajibu wa kuripoti kisheria
Data ya Utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Taarifa ya Malipo, Historia ya Kifedha, Taarifa ya Ajira, Taarifa ya Kujitolea
Wajibu wa Kisheria
Young Life iko chini ya wajibu fulani wa kuripoti kisheria na huenda kuripoti huku kujumuishe taarifa yako ya kibinafsi lakini tu kwa kiwango ambacho Young Life inaruhusiwa kisheria kusambaza taarifa hii.
Kupeleka bidhaa na huduma za Young Life
Data ya Utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Taarifa ya Malipo, Taarifa ya Young Life
Mkataba
Huenda utake kununua shati au kikombe kutoka kwenye duka letu la mtandaoni, au huenda utake kujiandikisha katika mashindano ya gofu.
Kuomba maoni kutoka kwako kuhusu shughuli, bidhaa na huduma za uchungaji za Young Life
Data ya Utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Maombi na Mapendeleo, Hati za Utambulisho wa Usalama, Demografia, Taarifa ya Young Life
Maslahi Halali
Huenda uombwe utoe maoni mara kwa mara kuhusu tukio ili tuendelee kujiboresha.
Kujibu maombi yako
Data ya Utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Maombi na Mapendeleo, Hati za Utambulisho wa Usalama, Demografia
Wajibu wa Kisheria
Tunatumia taarifa yako ya kibinafsi kujibu haraka ombi lolote ulio nalo kwa Young Life.
Kujibu malalamiko yako
Data ya Utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Maombi na Mapendeleo, Demografia
Wajibu wa Kisheria
Tunatumia taarifa yako ya kibinafsi kujibu haraka lalamiko lolote ulio nalo dhidi ya Young Life na kujibu haraka wasiwasi wowote kuhusu haki zako na taarifa ya kibinafsi.
Kuhakikisha sheria na masharti ya usalama wa watoto
Data ya Utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Taarifa ya Ajira, Taarifa ya Kujitolea
Wajibu wa Kisheria
Young Life hufanya uchunguzi wa historia ya uhalifu mara kwa mara na hojaji ya dereva kama sehemu ya kujituma kwetu katika viwango vya juu zaidi vya usalama wa watoto.
Kuendelea kuhusisha wanaopenda kuwa marafiki wa Young Life katika uchungaji wa Young Life unaoendelea
Data ya Utambulisho, Taarifa ya Mawasiliano, Maombi na Mapendeleo, Demografia, Taarifa ya Young Life
Maslahi Halali
Young Life ina mpango wa uchunganji unajitolea kuendelea kuwasiliana na wanafunzi wa zamani wa Young Life- Wanafunzi wa Zamani na Marafiki wa Young Life. Tovuti ya Wanafunzi wa zamani na Marafiki na mpango unakuruhusu ujiunge na watu wengine ambao wamejihusisha na wanajali kuhusu Young Life. Tovuti ya Wanafunzi wa zamani na Marafiki pia inatoa chaguo bora la kuamua kuacha mawasiliano.
Tunapata taarifa ya kibinafsi kukuhusu kwa njia zifuatazo:
Kwa kawaida Young Life huwa haifichui taarifa ya kibinafsi kwa mtu yeyote ambaye hayuko katika shirika. Hata hivyo, Young Life ni shirika la ulimwenguni ambalo huenda, kwa sababu zilizotajwa hapa juu, ipeane taarifa yako ya kibinafsi kwa:
Young Life ni shirika la ulimwenguni linaloendesha shughuli zake katika sehemu mbalimbali za dunia kupitia ofizi za tawi, tanzu, na mashirika. Kwa hiyo, huenda Young Life ihamishe taarifa yako ya kibinafsi kutoka nchi moja hadi nyingine. Watu wote walioko katika Eneo la Kiuchumi la Ulaya au Uingereza wanahitaji kujua kwamba huenda tuhamishe taarifa yenu ya kibinafsi nje ya Eneo la Kiuchumi la Ulaya au Uingereza kwa ajili ya uchakatishaji.
Uhamisho wowote wa taarifa ya kibinafsi kutoka katika nchi moja hadi nyingine utafanywa kwa vizuizi vipasavyo na kulingana na sheria zinazotumika. Young Life na tanzu na mashirika yake ya Ulaya yameweka masharti kwenye mkataba ili kudhibiti uhamishaji wa data kutoka katika nchi ya Ulaya hadi nchi nyingine, kama vile Marekani.
Ikiwa unaishi katika Eneo la Kiuchumi la Ulaya au Uingereza, una haki fulani zinazohusiana na taarifa yako ya kibinafsi. Ikiwa ungependa kutumia haki hizo zozote, tafadhali tumia Young Life barua pepe kwa privacy@younglife.org. Tutajibu ombi lako ndani ya siku 30. Huenda tuhitaji kuthibitisha utambulisho wako ili tushughulikie ombi lako.
Haki hizi za Ulaya ni:
Huku haki zilizoelezewa hapa juu hazihusu watu ambao wako nje ya Eneo la Kiuchumi la Ulaya na Uingereza, kama swala la haki na uhuru, bado tunajali maswali na wasiwasi wako unaohusiana na taarifa yako ya kibinafsi. Ikiwa hauishi katika Eneo la Kiuchumi la Ulaya au Uingereza, unaweza kuwasiliana na Young Life kwa privacy@younglife.org ili kutoa ombi linalohusiana na data yako ya kibinafsi.
Ili kuhifadhi na kulinda taarifa ambayo tunakusanaya, Young Life imetumia taratibu halisi zinazofaa, za kielektroniki na usimamizi ili kuzuia kufikia bila idhini na kudumisha usahihi wa data. Programu ya usimbaji fiche ya intaneti, itifaki ya Tabaka la Soketi Salama (SSL), inatumiwa kulinda urushaji wa data nyeti kwenye benki au maelezo ya kadi ya mkopo. Ikoni ya kifuli iliyoko chini ya dirisha la kivinjari chako au mstari wa buluu uliopo kando ya dirisha unaashiria kwamba tovuti ni salama. Wakati mwingine ulinzi wa nenosiri unatumiwa kulinda faragha na usalama wako. Young Life itaendelea kuongeza taratibu za usalama za sasa na kuchukua itifaki mpya za usalama zinazohitajika kutimiza kiwango cha utunzaji ambao tumeahidi katika sera zetu na katika Kauli hii ya Faragha.
Young Life pia imejituma katika kujibu haraka unaoweza kuwa uvunjaji wa data na imeweka Mchakato wa Itifaki ya Uvunjaji wa Data inayojumuisha notisi za wakati unaofaa kama inavyohitajika na sheria inayotumika.
Huenda tovuti za Young Life zitumie vidakuzi kukutambua na huenda zikuruhusu uingie kiotomatiki bila kujaza tena jina lako la mtumiaji na nenosiri kila wakati unapotembelea tovuti yetu. Vidakuzi vimefichwa na havihifadhi taarifa yoyote inayoweza kukutambua, kama vile jina lako la mtumiaji, nenosiri au anwani ya barua pepe. Ikiwa vidakuzi havijaruhusiwa kwenye kivinjari chako, huenda bado uweze kutumia tovuti ya Young Life, lakini utahitajika kuingiza nenosiri lako kila wakati unapotembelea tovuti.
Kwa kawaida, tovuti za Young Life ni tovuti za kielimu kwa wazazi na watoto kuhusu Young Life. Tunataka kutoa mazingira salama, ya burudani ambapo watoto na wazazi wao wanaweza kugundua Young Life, klabu yao wenyewe ya Young Life na shughuli nyingine za Young Life. Hakuna yoyote kati ya tovuti za Young Life ambazo huchukua taarifa ya kibinafsi kwa maksudi kutoka kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 13, isipokuwa ambapo taarifa ya kibinafsi lazima ichukuliwe kutoka kwa watoto na/au wazazi ili kurahisisha kushiriki katika matukio na shughuli za Young Life.
Tunajali kuhusu faragha ya watoto na huwa tuko makini sana kuhifadhi taarifa za kibinafsi za watoto wote. Hatuhitaji mtoto atupatie taarifa yoyote ya kibinafsi mbali na inayohitajika ili kushiriki katika shughuli maalum, na huwa hatuwekei ushiriki wa mtoto masharti ili afichue taarifa zaidi ya kibinafsi inayohitajika ili ashiriki katika shughuli. Taarifa zote za kibinafsi tunazokusanya zinaweza tu kufikiwa na wafanyakazi na watu waliojitolea na waliodhinishwa wa Young Life, na watu pekee ambao wanahitaji kufikia taarifa ndio wanaoweza kuona taarifa hii kwa sababu zilizotajwa hapa juu. Tunafanya kazi kwa bidii kulinda usiri, usalama na uadilifu wa taarifa hiyo.
Kama uchungaji kwa watoto, Young Life imejituma sana katika usalama na ustawi wa watoto. Tunazo sera na taratibu zilizoundwa ili kuhakikisha kwamba sheria za faragha zinazotumika zinafuatwa na kufanya matendo bora yanayokubalika, hasa kwa vile inahusu notisi na idhini ya wazazi. Wazazi wana haki ya kuomba kwa wakati wowote kwamba taarifa iliyokusanywa kuhusu mtoto wao iondolewe kutoka kwenye mitandao na hifadhidata ya Young Life. Unaweza kuwasiliana na Young Life kwa privacy@younglife.org.
Wakaazi wa California wanaotoa taarifa ya kibinafsi katika kupata bidhaa au huduma ili wazitumie wenyewe au watu walio nyumbani mwao wazitumie wana haki ya kuomba na kupata kutoka kwetu, mara moja, habari ya kalenda ya mwakani kuhusu maelezo ya mteja tuliyopeana, ikiwa yapo, kwa biashara nyingine ili wayatumie kwa uuzaji wa moja wa moja. Ikiwa inahusika, maelezo haya yanaweza kuwa kategoria za taarifa ya wateja na majina na anwani za biashara hizo ambazo tulipea maelezo ya wateja kwa mwaka wa kalenda uliopita hivi karibuni.
© 2004-2023 Young Life. All rights reserved.